THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Waziri wa Afya Mhe. Jenesta Mhagama (Mbunge) amefanya uteuzi na kuzindua Baraza jipya la Uuguzi na Ukunga Tanzania(TNMC) lenye jumla ya wajumbe 12 baada ya wajumbe wa Baraza la awali kumaliza muda wao.

Uteuzi wa wajumbe 12 wa Baraza ni kwa Mujibu wa kifunga namba 5 – (1) cha Sheria iliyotungwa na Bunge ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 ambacho kimempa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Afya kufanya uteuzi wa wajumbe wa Baraza.

Akizungumzana katika hafla ya uzinduzi amewataka wajumbe hao kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Baraza kuhakikisha wanasimamia, wajibu, weledi na kudhibiti wanotaka kuvunja Sheria, kanuni na taratibu za sekta ya Afya kupitia taaluma ya Uuguzi na Ukunga.

Kama serikali hatutamani kusikia muuguzi au Mkunga amavunja taratibu katika kutekeleza majukumu yake kwa sababu huyo mmoja anaharibu image ya wauguzi na wakunga wote, kwa hiyo mmepewa heshima ili ninyi mtusaidie na pale mtakapotakiwa kufanya dhidi ya wale wanaoharibu heshima na sifa ya taaluma yetu, muongozwe na uzalendo kwa maslahi ya jamii nzima ya Watanzania.
wajumbe wapya watahudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu tangu kuteuliwa kwao.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TMNC ni mamlaka ya kisheria inayosimamia wanataaluma na taaluma za uuguzi na ukunga Tanzania, Chini ya Sheria ya Uuguzi na ukunga ya mwaka 2010 na kanuni zake (The Nursing and Midwifery Act 2010) ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini zinakiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.