Msajili wa baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania anapenda kuwatangazia Wananchi wote kuwa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linatimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake.
Kuelekea Sherehe za Maadhimisho hayo kutakuwa na maonyesho na huduma mbalimbali za Kiuuguzi zitakazotolewa kuanzia tarehe 17/3/2023 hadi tarehe 19/3/2023 katika viwanja vya Nyerere square Jijini Dodoma.
File Type:
pdf