THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limeweka kambi ya siku sita mkoani Geita kwa lengo la utoaji Mafunzo ya Maadili na sheria ya Uuguzi na Ukunga kwa wauguzi na wakunga katika Halmashauri zote Mkoani humo.

Ziara hiyo ya kawaida inalengo la kutoa elimu ya Maadili na Sheria kwa wauguzi na wakunga ili kuendelea kutoa Huduma kwa kuzingatia Maadili, Sheria, kanuni na taratibu ili jamii iweze kupata Huduma bora na Salama.

Aidha, Akitoa mafunzo hayo katika halmasahauri ya Nyang’wale Mkoani Geita Msajili wa baraza hilo Bi.Agnes Mtawa amewapongeza wauguzi na wakunga Nchini kwa utoaji huduma bora kwa jamii, huku akibainisha kuwa takribani asilimia 60 hadi 80 ya watoa huduma za Afya Nchini, ni wauguzi na wakunga, hivyo ni vyema wakapata Mafunzo hayo ili kuendelea kuboresha zaidi Huduma za Afya Nchini.

Kwa Upande wake Mwanasheria wa Baraza Bwana George Shilla, amewataka wauguzi na wakunga kujitokeza katika vituo vilivyopangwa kwaajili ya mafunzo hayo ili kuijua vyema Sheria hiyo ambayo inaiongoza Taaluma ya Uuguzi na Ukunga Nchini.

Naye Bi. Mwajuma Mutabazi, ambaye ni muuguzi mbobezi kutoka Baraza amesema, ili kuwa muuguzi na mkunga mzuri ni vyema kuzingatia maadili ya taaluma hiyo huku ukitanguliza Utu katika utoaji Huduma.

Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni Mamlaka ya Kisheria iliyoanzishwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na Kanuni zake, kwa lengo la kusimamia wanataluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga, ili kuhakikisha jamii inapata Huduma za Afya zilizo bora na Salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *