Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania leo Tarehe 03 Oktoba 2023 limeketi katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwa ajili ya kikao cha cha robo ya kwanza cha mwaka wa Fedha 2023/2024.Kikao hiki cha kikanuni, katika utendaji kazi wa Baraza, kinaangazia agenda 14 ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa kazi katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 kutoka katika Kurugenzi, Divisheni na Vitengo.