Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) linatangaza Matokeo ya Mtihani wa usajili na leseni uliyofanyika tarehe 07.09.2023 Matokeo hayoyanapatikana kwenye akaunti ya kila Mtahiniwa kwenye mfumo wa Baraza (hppts://ww.tnmcis.go.tz).
Matokeo haya yamechelewa kutangazwa kutokana na baadhi ya watahiniwa kukiuka taratibu za ufanyaji Mitihani ambazo zilizosababisha kufanyika uchunguzi ili kubaini chanzo cha ukiukwaji huo.
Baraza limekamilisha uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na hivyo kufikia maamuzi yafuatayo:-
- Kutoa Matokeo ya Mtihani kwa ngazi ya Shahada na Astashahada kwa kuwa hakuna Ushahidi wa ukiukwaji wa taratibu za Mtihani.
- Kufuta Mtihani wa ngazi ya Stashahada (Diploma) baada ya kubaini ukiukwaji wa taratibu za Mtihani.
- Watahiniwa wote waliofutiwa Mtihani wa ngazi ya Stashahada (Diploma) watarudia Mtihani katika tarehe watakayotangaziwa, hivyo wanashauriwa kufanya maandalizi ya Mtihani huo wa Marudio na hakutokuwa na malipo yoyote kwa Watahiniwa wa Mtihani wa marudio.
- Kwa wale wa Shahada na Astashahada ambao hawakufaulu watatakiwa kurudia Mtihani huo kwa utaratibu wa kawaida.
- Waliofaulu Mtihani wa Shahada na Astashahada watasajiliwa kwa mujibu wa utaratibu.
Hata hivyo Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa amewataka Watahiniwa wote kufuata Taratibu, Kanuni za Mitihani na kuacha njia za mikato ambazo hazina tija na huleta usumbufu usiokuwa wa lazima.