THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Search

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeandaa Mahafali kwa Wahitimu wa kozi za Uuguzi na Ukunga waliofaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 07.9.2023.

Mahafali hayo ya tisa yamefanyika Jijini-Dodoma, ambapo wauguzi na wakunga wapatao 81 wametunukiwa vyeti pamoja na leseni za kutambuliwa rasmi kama wataalam wa kada hizo.

Akizungumza wakati wa utoaji wa leseni za kitaaluma na Vyeti, Mgeni rasmi ambaye ni Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa, amewapongeza wauguzi na wakunga hao kwa hatua waliyoifikia ya kuaminiwa na Baraza na kuwataka kwenda kuhudumia jamii kwa kutanguliza Utu.

“Tujikite katika kutoa Huduma bora kwa jamii, leo Baraza limeridhika na kiwango cha taaluma yako kwa kukupa leseni na cheti cha usajili wa Taaluma Mkaihudumie jamii kwa kufuata Sheria ya Uuguzi na Ukunga “-Bi.Agnes Mtawa

Kwa Upande wake Mwanasheri wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Erasto Shilla, amewasihi wauguzi na wakunga kuzingatia Sheria ya Uuguzi na Ukunga wanapokuwa kazini ili kuepukana na adhabu ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria.

Watahiniwa wa waliohitimu katika Mahafali hayo ya tisa ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni 81, ambapo ngazi ya Astashahada ni 32 na upande wa Shahada wakiwa ni 49.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania chini ya Sheria ya Mwaka 2010 na kanuni zake (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa wateja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *