THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeendesha Mafunzo ya namna ya kushiriki utoaji huduma katika chumba cha upasuaji kwa wauguzi na wakunga katika Hospitali ya Mirembe Jijini Dodoma.

Akitoa mafunzo hayo Afisa Muuguzi Mbobezi Kitengo Cha Upasuaji Bi. Salome Kassanga amewataka watumishi kuyazingatia yale waliyoyapata kutoka katika mafunzo hayo ili kuhakikisha jamii inapata huduma iliyo bora na salama.

Kwa upande wake Muuguzi Kiongozi katika chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Mirembe Bi. Devotha Kimambo amelipongeza Baraza kwa Mafunzo hayo kuwa yatasaidia kuboresha mazingira ya vyumba vya upasuaji na kuwaongezea ujuzi watumishi hao

Nao washiriki wa Mafunzo hao amemshukuru Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa kwa jitihada za utoaji wa mafunzo ya aina hiyo kwa watumishi waliopo kazini huku wakiiomba serikali irudishe mafunzo hayo yaliyositishwa ili kuboresha utoaji wa huduma ya aina hiyo kwa wateja mbalimbali.

Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na wauguzi na wakunga yanatarajiwa kuwa chachu ya utoaji wa huduma bora Hospitali ya Mirembe Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *