THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika Tarehe 29.12.2024.

Akitangaza Matokeo hayo katika Ofisi za Baraza Jijini Dodoma, Msajili wa Baraza Bi.Agnes Mtawa, amesema, Mtihani huo uliofanyika katika vituo nane (8) ambavyo ni Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Tandabui-Mwanza, Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi-Mbalizi, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu Stephano Moshi-Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana (St.John) – Dodoma, Chuo Kikuu cha Kampala-Dar es Salaam, Chuo cha Biashara -Dodoma (CBE) na Chuo cha Tabora Polytechnic.

Jumla ya watahiniwa 2099 (50.7%) walifaulu mtihani huo kati yao watahiniwa 346 (72%) ni ngazi ya Shahada ya Uuguzi, 1737 (48%) ni Stashahada ya Uuguzi na Ukunga na watahiniwa 16 (30.8%) ni Astashahada ya Uuguzi na Ukunga.Watahiniwa 2043 (49.3%), walifeli mtihani huo, kati yao 136 (28%) ni ngazi ya Shahada (Digree) ya Uuguzi, 1871 (52%) ni Stashahada (Diploma) ya Uuguzi na Ukunga na 36 (69.2%) ni Astashahada( Cheti) ya Uuguzi na Ukunga.

“Maswali ya mtihani huu yalichambuliwa kwa ngazi ya mafunzo ili kuona hali ya ufaulu wa watahiniwa katika maeneo ya umahiri uliopimwa kwa kuzingatia orodha ya vipimo vya umahiri na watahiniwa wengi walionekana kushindwa na kuwa nauelewa mdogo katika maeneo ya Misingi ya Uuguzi (Basic/ Fundamentals of nursing), tiba upasuaji na magonjwa ya dharura na mahututi (Medical Surgical Nursing and intensive care), Afya ya mama na mtoto (Midiwifery and Child Health), Afya ya Akili (Mental Health Nursing)” alitanabaisha Msajili huyo.

Aidha, ameongeza kuwa, Katika Mtihani huu, hali ya Ufaulu inaonesha kunaongezeko la asilimia 4.7 ukilinganisha na mtihani uliofanyika mwezi Disemba, 2022 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 4.6. Ngazi ya Shahada ni 71%, Ngazi ya Stashahada ni 71% Ngazi ya Astashahada ni 56%
Akihitimisha tarifa yake, Msajili Mtawa, amesema, Baraza litatoa mrejesho kwenye vyuo vya Uuguzi na Ukunga na vituo vya utarajali kuendelea kuongeza usimamizi wanafunzi ili kujifunza zaidi katika maeneo hayo.

Baraza kwa kushirikiana na viongozi wa Uuguzi na Ukunga katika Mikoa na Wilaya (Supervisory Authority) kuendelea kuimarisha ufuatiliaji wa vyuo vya Uuguzi na Ukunga na usimamizi wa wanafunzi katika maeneo ya kujifunza kwa vitendo

Baraza kufuatilia vyuo vya Uuguzi na Ukunga ili kubaini hali halisi ya uwepo wa mazingira ya ufundishaji katika hospitali na vyuo.
Kufanya ufuatiliaji wa vituo vya mafunzo ya utarajali na vyuo ambavyo watahiniwa wameonyesha kupata ufaulu wa kiwango cha chini ili kubaini changamoto zinazowakabili.

Wauguzi na wakunga hao wanatarajiwa kukabidhiwa chei cha usajili na leseni zao za kutambuliwa kwanye Mahafali maalum ya kitaaluma yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dodoma 23/02/2024

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *