THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Search

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ametoa pongezi hizo wakati wa ufunguzi wa Mkutano. ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC ukiwahusianisha watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ambao unafanyika Jijini Mwanza ambapo Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania wakiwa ni sehemu ya wadhamini wa mkutano huo.

Mkutano huo uliobebwa na kauli mbiu ya “Vyombo vya Habari na Falsafa ya 4R” ikiwa na maana ya Mageuzi,maridhiano, ushahimilivu na kulijenga Taifa kwa kila Mtanzania kushiriki ili kulijenga Taifa letu.

“Tumieni Mkutano huu kujifunza mambo muhimu kwa ajili ya kuhabarisha umma hasa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, ndio maana Serikali inaona kuna umuhimu wa kila idara ,Taasisi za Umma ziwe na Maafisa habari ili kuupa Umma taarifa hasa kujibu kero za wanajamii”-Waziri Nape.

Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania kimeshiriki Mkutano wa Mafunzo wa watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia TBC ambapo Ezekiel M Nyalusi Afisa Uhusiano TNMC, amepokea Cheti cha pongezi ya udhamini wa mkutano huo kwa niaba ya Baraza.

Mada mbalimbali zinazo husu utayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma zimetolewa katika mkutano ambao utatamatika tarehe 23 mwezi huu 2024.

Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni Mamlaka ya Kisheria iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya 2010, na Kanuni zake kwa lengo la kuhakikisha huduma zitolewazo na wauguzi na wakunga zinaubora na salama kwa wateja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *