Wauguzi na wakunga wapya wapatao 2099 wamekula kiapo cha kuitumikia taaluma hiyo kwa kuzingatia maadili, miiko, sheria na kanuni za uuguzi na ukunga.
Wamefikia hatua hiyo baada ya kufaulu mtihani wa Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) uliofanyika Desemba 29, 2023 na hivyo kupata sifa za kuorodheshwa, kusajiliwa na kupewa leseni za kutambuliwa rasmi kama wataalamu wa kada ya uuguzi na ukunga nchini.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Tumaini Nagu ameshuhudia leo jijini Dodoma wauguzi hao na wakunga wakiapishwa katika mahafali ya 10 ya Kitaaluma yanayoratibiwa na TNMC.
Kati yao, 346 ni wa shahada ya kwanza, 1737 ni ngazi ya stashahada huku 16 wakiwa ni ngazi ya astashahada.