THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadili kutoka TNMC Bi. Jane Mazigo amewataka Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini kusimamia vyema huduma za Afya nchini sambamba na kuhakikisha huduma ya Uuguzi na Ukunga zinafuata Maadili, taratibu na miongozo ya huduma ya Afya.

Hayo ameyasema wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazojali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

Mkutano huu unafanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa PSSSF tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *