THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa, amewapongeza wauguzi viongozi kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika utendaji wa majukumu ya Baraza katika maeneo yao ya kazi.

“Nitumie fulsa hii kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayoifanya huko kwenye maeneo yenu ninyi ni wasaidizi wangu, fanyeni kazi kupunguza malalamiko ya wateja pia simamieni vyema wauguzi watarajali na wale wanao wabeza waleteni huku Barazani tutawashughulikia kwa mujibu wa Sheria”-

Bi.Mtawa ametoa pongezi hizo wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinajali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

Mkutano huu unafanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024 Umebebwa na Kauli mbiu “Huduma sitaha na mawasiliano Madhubuti ni wajibu wa kila mtoa huduma za Afya”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *