THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania(TANNA) Bwana Alexanda Balulya, amesema kuna umuhimu wa kushirikiana katika utendaji kazi wawapo vituo vya kazi na kuiheshimu tasnia ya Uuguzi na Ukunga nchini. “Ubaguzi wakitaaluma hautakiwi katika utendaji kazi, tutunziane heshima na mapungufu ya kitaaluma huku tukiitatua migogoro midogo midogo katika tasnia yetu tusikimbilie kwenye vyombo vya habari” amesema Bwana Balulya.

Ameyasema hayo Rais wa TANNA akichangia hoja wakati wa Mkutano wa mwaka wa wauguzi viongozi wa Mikoa, Halmashauri, Hospitali ya Taifa, Hospitali za Kanda, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali maalum, wauguzi wakufunzi kutoka Vyuo vikuu na Vyuo vya kati ulioandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Lengo la Mkutano huu ni kuwaleta pamoja Wauguzi viongozi kutoka ngazi zote za kutolea huduma za Afya chini na wadau mbalimbali wa Afya kujadili na kupanga mikakati ya pamoja ya namna bora ya kuondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuhakikisha huduma zinazojali utu, heshima, upendo na mawasiliano madhubuti baina ya mtoa huduma na mteja zinatolewa, pia kuweka mikakati ya kuimarisha usimamizi wa wanafunzi wauguzi katika maeneo ya kutolea huduma za Afya.

Mkutano huu unafanyika Jijini Dodoma katika kuanzia tarehe 18/03/2024 hadi 20/03/2024 Umebebwa na Kauli mbiu “Huduma Sitaha na Mawasiliano Madhubuti ni wajibu wa kila mtoa huduma za Afya”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *