THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Search

Bi.Salome Kassanga Mkufunzi wa Mafunzo ya chumba cha Upasuaji na Afisa Mwandamizi kutoka TNMC ameyasema hayo wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na uongozi wa mkoa wa Pwani, wakishirikiana na wadau wa Shirika la Korea Foundation for International Health Care (KOFIH) wakiwa na lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na watoto wachanga.

“Ni muhimu kufuta taratibu za chumba cha Upasuaji kuepuka maambukizi kutokana mpangilio mzuri wa chumba cha upasuaji, Mazingira Rafiki hasa vifaa viwe safi muda wote” alisema Bi Kassanga.

Kwaupande wake muwezeshaji Dokta Alfonce Moyo Kutoka hospitali ya Tumbi amebainisha umuhimu wa kushirikiana kama timu wakati wautoaji huduma katika chumba cha upasuaji na kusema ushirikiano huo unaleta tija na ufanisi wa utendaji kazi hasa kwenye chumba cha upasuaji.

“Mara nyingi watu hawafahamu suala la utoaji huduma katika chumba cha upasuaji wanadhani anahusika Daktari pekee, kumbe asilimia kubwa Muunguzi ndiye wa kwanza kuandaa mazingira yote ya huduma hii lakini mimi niseme kitu hapa ni muhimu umma ukafahamu kuwa sisi tunafanya kazi kama timu, mteja yule ni wetu sote hivyo kila mmoja wetu anajukumu la kumuhudumia ipasavyo hivyo mafunzo haya yataleta sura mpya ya kushirikiana kikamilifu katika utoaji huduma hii” alisema Dkt. Moyo

Naye, Dkt. Tanya Mahalo, Mtaalamu wa dawa ya Usingizi na ganzi kutoka hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, amesema ni vyema kuanza kumuandaa mgonjwa nje ya chumba cha upasuaji kwa kumpa taarifa sahihi ya huduma ipi anayoenda kuipokea, na baada ya kupata huduma lazima awe chini ya uangalizi maalumu mpaka atakapo pata nafuu, ameongeza kuwa ni vizuri tukamuhudumia mteja kwa upendo hasa awapo katika kituo cha kupokea huduma.

Mafunzo yameanza tarehe 08 Aprili 2024 na yanatarajiwa kutamatija tarehe 04 Mei 2024 katika Halmashauri ya Wilaya Kibaha DC, Kibaha TC, Kisarawe, Kibiti na Rufiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *