THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Wauguzi na wakunga wapya 415 wametunukiwa vyeti na usajili na leseni katika Mahafali ya 11 ya kitaaluma  jijini Dodoma.

Akifungua Mahafali hayo Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Prof. Lilian Msele ameipongeza Menejimenti ya Baraza kwa maandalizi ya mahafali hayo huku akiwataka wauguzi na wakunga wapya kwenda kuitumikia jamii kwa kufuata sheria, miongozo na taratibu.

Katika hatua nyingine Prof. Msele amewataka wauguzi viongozi kusimamia vyema huduma za Uuguzi na Ukunga hapa nchini

”Hivi siku za karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya wateja juu ya huduma za Uuguzi na Ukunga, Nitumie fulsa hii kuwataka wauguzi viongozi kusimamia vyema maadili kwa wauguzi na wakunga hapa nchini ili kuweza kupunguza malalamiko mengi ya wateja katika jamii” alisema Prof Mselle.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga Tanzania na Muuguzi Mkuu wa Serikali Bi. Ziada Sellah amewapongeza wauguzi na wakunga wapya kwa kuhitimu masomo na amekaribisha katika kada ya Afya huku akiwataka kuendelea kuzingatia maadili ya taaluma.

“Nipenda kauli mbiu inayosema Wauguzi na wakunga ni watu maalumu kwa kazi maalum, hivyo tujivunie taaluma yetu, sasa mmemaliza kupewa leseni na baraza mimi nawapokea katika kada ya Afya ila mkifanya makosa ya kitaaluma mimi nitawarudisha kwenye baraza” alisema Bi. Lilian

Naye Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadli Bi. Jane Mazigo amebainisha idadi ya wauguzi na wakunga waliosajiliwa na kupewa leseni ni wamefikia 52,188 hapa nchini huku baraza liliendelea kusimamia huduma za Uuguzi na Ukunga nchini ili jamii iweze kupata huduma iliyobora salama.

Hata hivyo, Baadhi ya wauguzi na wakunga wameahidi kwenda hudumia jamii kwa kufuata sheria taratibu na miongozo yote ya Afya hapa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *