Wafanyakazi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) wameshiriki Katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo inasema “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao bora na kinga Dhidi ya hali Ngumu ya Maisha”
Hata hivyo Maadhimisho ya wafanyakazi kitaifa yanafanyika Mkoani Arusha ambapo Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.