THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wauguzi kula kiapo cha utoaji wa huduma bora ikiwa ni pamoja na kuwapa wagonjwa faraja na msaada wa saikolojia.”Msiondoke hapa mpaka mle kiapo cha kutoa huduma bora kwa niaba ya wauguzi wengine wote walioko kwenye vituo vya kutolea huduma na mkakitendee haki kiapo kwa kufanyakazi kwa moyo na kwa mapenzi yote kwa watanzania,” amesema.

Amesema wagonjwa wanakuwa hospitalini wanahitaji faraja na msaada wa saikolojia kwa kupokelewa vizuri na kupewa maneno mazuri ili apate unafuu.

“Lakini wengine wenu hawana kauli nzuri, hawawasikilizi wagonjwa mpaka wapewe fedha hii sio afya, kwa taaluma yenu nataka niwaone mkila kiapo cha utoaji wa huduma bora.”

Waziri Mchengerwa alimuekeza Katibu Mkuu – TAMISEMI kuhakikisha anafanyia kazi changamoto za wauguzi zilizowasilishwa ikiwemo ile ya muundo kwa wauguzi na upandaji wa madaraja.

“Haiwezekani watu mfanyekazi ya kujitoa halafu hata madaraja hampandishwi, hii si sawa sasa naelekeza changamoto hii ifanyiwekazi na mwakani tutakapokutana tena iwe imeshafanyiwa kazi.”

Awali akiwasilisha taarifa ya Wauguzi hao Katibu Mkuu wa chama cha Wauguzi Tanzania Bw. Samson Mwangoka amesema wauguzi wana changamoto ya kutopandishwa madaraja, muundo usiotoa kipaumbele kwa taaluma na kutokuwa na bajeti.

Waziri Mchengerwa amefungua Kongamano la kisayansi na Mkutano Mkuu wa 51 wa Chama Cha Wauguzi Tanzania ambapo mkutano huo utaambatana na maadhimisho ya siku ya wauguzi dunia tarehe 12 may mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *