THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Menejimenti ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) leo June 06, 2024 imefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Ofisi ya Baraza (site visiting) kuangalia hatua za ujenzi wa Ofisi za Baraza.

Ujenzi huo unaotekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Strategic Business Solution Limited (SBS) unaendelea katika eneo la Medeli Jijini Dodoma ambapo hadi sasa umefikia asilimia 52% huku ukitarajiwa kukamilika tarehe 16.08.2024, ukigharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 za kitanzania.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linajenga Ofisi Kuu Jijini Dodoma hii ni baada ya maelekezo ya Serikali ya kuzitaka Taasisi zote za Umma kuhamia Makao Makuu ya nchi, awali Ofisi kuu za TNMC zilikuwa Mjini Kibaha mkoani Pwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *