Ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, inawatangazia wahitimu wote wanaotarajia kufanya mtihani wa Usajili na Leseni, kuwa mtihani unatarajiwa kutafanyika tarehe 23/08/2024.
Kwamba, Dirisha la maombi limefunguliwa lipo wazi toka tarehe 01/07/2024 na litafungwa tarehe 14/08/2024. Maombi yote yafanyike kupitia mtandao kwa kutumia mfumo wa Baraza www.tnmcis.tnmc.go.tz
Waombaji wote mnajulishwa kuzingatia yafuatayo;
- Kuwa na namba ya utambulisho (Indexing Number) kwa mujibu wa kifungu cha 14 (1) cha kanuni za mafunzo.
- Kuzingatia taratibu zote za maombi ambazo zimeambatanishwa ikiwa ni pamoja na kuweka picha sahihi (Passport Size 45X35), kujaza majina sahihi yanayoendana na vyeti vya kufunzu elimu ya Sekondari.
- Kufanya malipo kwa wakati na kuchagua kituo sahihi cha mtihani.
Mtihani utafanyika katika vituo vinne (4) ambavyo ni chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Jijini Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) Jijini Mwanza, Taasi ya Uhasibu Mbeya, Jijinini Mbeya na Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Jjijini Dar es Salaam.