THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Mapema Julai 28, 2024 ameongoza mamia ya Wanariadha kwenye mbio za NBC Marathoni zilizoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC Bank).

Mbio hizo za Kilomita 42, 21, 10, 5 na Mbio maalum za Viongozi zimeanzia viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma na kuishi katika viwanja hivyo ilihali Shabaha yake ikiwa ni kuchangia uboreshaji wa huduma za Afya nchini, ambapo Shilingi za kitanzania Milioni 100 zitapelekwa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road, Millioni 100 kutumika kusomesha wauguzi na wakunga kupitia Taasisi Benjamini Mkapa na Milioni 50 kuchangia ujenzi wa Majengo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mbali ya michango hiyo mbio hizo zinatumika kuhamasisha mazoezi ili kupambana na Magonjwa yasiyoambukiza.

Baadhi ya Viongozi walioambatana na Waziri Mkuu ni pamoja na Naibu Waziri wa Michezo Sanaa na Utamaduni Mhe. Hamiss Mwinjuma, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt John Jingu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Mohamed Janabi, Mkurugenzi wa Huduma za kinga Ntuli Kapologwe pamoja na mamia ya wananchi kutoka ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ni miongoni mwa taasisi iliyoshiriki katika marathon kwa kuwalipia ada za ushiriki wauguzi na wakunga zaidi ya 90 kushiriki zoezi hilo.