Akizungumza na vyombo vya Habari katika Maonesho ya kimataifa ya Nanenane Jijini Dodoma Afisa Uhusiano Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) Ndugu Ezekiel Nyalusi amesema jamii ni vyema ikafahamu haki na wajibu wa mteja au mgonjwa pindi anapofika kupewa huduma za Afya katika kituo cha kutolea huduma.
Ndugu Nyalusi amzeiainisha haki hizo kuwa ni: Kupatiwa taarifa unazohitaji kuhusu ugonjwa na matibabu yako. Kupatiwa matibabu bila kukemewa, kukaripiwa au kufedheheshwa,Kupata huduma kwa wakati, kutegemea aina ya huduma, Kuwa na hiyari kupata taarifa zako za kiafya, Kupata huduma stahiki kwa makundi maalumu kama vile, Walemavu, Wazee, Wajawazito, Watoto wa chini ya miaka mitano na wenye magonjwa sugu, kutoa mrejesho wa huduma uliyopatiwa, Kufuata kanuni na taratibu za kituo husika, Kuwaheshimu watoa huduma ikiwa ni pamoja na kutumia lugha Safi, Kumueleza muhudumu wa Afya taarifa zote ambazo zitamuwezesha kutoa tiba sahihi ikiwa ni pamoja na kumpa rekodi za matibabu ya awali ulizonazo na Kutafuta matibabu kwa haraka na mapema iwezekanavyo ili wahuhudumu wa Afya waweze kukupa huduma sahihi.
Kwa Upande wake Bi. Irene Chilewa ambaye ni Kaimu mkuu kitengo cha Udhibiti Ubora TNMC amewataka wauguzi na wakunga kufuata Kanuni za Maadili ya Uuguzi na Ukunga Tanzania kuwa ni Kuheshimu Utu uhai, kupata idhini ya mteja kabla ya kutoa huduma, kutimiza wajibu wako na kuwa tayari kuwajibika kwa matendo yako, kudumisha weledi na ujiendeleze kitaaluma,kuwa mwaminifu na kutoa huduma bila upendeleo, kushirikiana na watoa huduma wengine na kufanya kazi kama timu, kutunza siri za Mteja/ Mtu unaye mhudumia.
TNMC imeshiriki Maadhimisho ya maonesho ya kitaifa ya Nanenane kwa muda wote wa siku nane ikitoa huduma mbalimbali za Baraza kama vile Uhuishaji wa leseni, sajili na utoaji wa elimu ya sheria na maadili kwa wauguzi na wakunga na kutoa elimu ya haki ya mteja akiwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya