THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Search

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msajili TNMC Bi. Agnes Mtawa imeeleza kuwa Mtihani wa usajili na leseni unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2024. TNMC imefunga dirisha la usajili kwa watahiniwa wenye sifa za kufanya Mtihani huu, ambao hufanyika  kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya  mwaka 2010 Kifungu 6 (o) kwa lengo la kupima umahiri kabla ya kumruhusu mwanataaluma kwenda kutoa huduma kwa jamii.

Taarifa ya msajili imeeleza kuwa Katika usajili wa watahiniwa ulioanza 01 Julai 2024 nakufungwa 14 Agosti 2024. Jumla ya watahiniwa 3,099 wamekidhi vigezo na wamesajiliwa kufanya mtihani huu. Watahiniwa hawa wanajumuisha ngazi ya Shahada 195, Stashahada 2823 na Astashahada 81.

Bi. Mtawa katika taarifa hiyo amevitaja Vituo vya Mtihani ni kama ifuatavyo;

  1. Chuo Kikuu cha Dodoma, (College of Business – Administration And School of Law (Humanities Bondeni) Kumbi ni CAFE THEATRE 1,2,3) UDOM kilichopo Jijini Dodoma
  2. Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Mbeya iliyoko Jijini Mbeya
  3. Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT) kilichopo Malimbe Jijini Mwanza
  4. Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) kilichopo Temeke jijini DSM

Aidha katika hatua nyingine Msajili amewataka Watahiniwa wote kufika siku moja kabla ya siku ya mtihani yaani Alhamisi ya tarehe 22/08/2024 katika vituo walivyochagua kuanzia saa mbili kamili asubuhi kwaajili ya maelekezo muhimu. Siku ya ijumaa ya tarehe 23/08/2024 kila mtahiniwa anatakiwa awe amefika kwenye kituo alichochagua 07:00 asubuhi bila kukosa na ambaye hatafika atakuwa amepoteza sifa ya kufanya Mtihani. Kila Mtahiniwa anatakiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani akiwa na muonekano nadhifu na vifaa vifuatavyo:

  1. Kalamu Nyeusi (aina ya Obama) au Penseli (HB Original)
  2. Picha mbili (passport size)
  3. Kitambulisho (Indexing card,) Kwa wale wasio kuwa na Indexing kadi wanatakiwa kuja na kitambulisho cha taifa au cha mpigakura.

Hata hiyo, Watahiniwa wanakumbushwa kuzingatia taratibu zote za mtihani na kuheshimu maelekezo ya wasimamizi uwapo chumba cha Mtihani. Pia, kujiepusha na tabia za udanganyifu kabla ya Mtihani, ukiwa katika chumba cha Mtihani na hata baada ya Mtihani, kwani ukibainika unajihusisha na udanganyifu wowote ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na kwa Mujibu wa Sheria hii adhabu yake ni kufutiwa mtihani   kwa Mujibu wa Kifungu 22 cha Kanuni.

Mwisho; Msajili Kwa niaba ya Baraza amewatakia Safari njema watahiniwa wote kuelekea kwenye vituo vya Mtihani na amewatakia Mtihani Mwema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *