THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), limetoa mafunzo elekezi kwa Madaktari, wauguzi,wakunga na wauguzi wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi wanaofanya kazi katika vyumba vya upasuaji pamoja na baadhi ya watumishi kutoka vitengo mbalimbali vya kutolea huduma wapatao 45 katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini, juu ya namna bora ya kutoa huduma katika chumba cha Upasuaji “Theatre Management” kwa lengo la kumlinda mgonjwa kuwa salama baada ya upasuaji.

Mafunzo yanayodumu kwa muda wa siku 14 yanaongozwa na Afisa Muuguzi Mbobezi kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Salome Kassanga akisaidiana na Muuguzi mbobezi katika chumba cha upasuaji Bi Happiness Liya kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Ligula.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mwezeshaji kutoka Baraza la Uuguzi na Ukunga amesema kuwa, lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Madaktari, Wauguzi, Wakunga na Wataalamu wengine katika chumba cha Upasuaji ili kuboresha huduma kwenye chumba cha Upasuaji na kukidhi viwango vya Kimataifa. “Tunatoa mafunzo haya ili kuhakikisha kuwa vyumba vya upasuaji kunakuwa na misingi bora ya usimamiaji na uendeshaji, misingi ya kudhibiti maambukizi kwa wagonjwa (IPC), uzingatiaji wa Maadili, Sheria, kanuni na miongozo katika chumba cha upasuaji, uvaaji wa sare maalumu za chumba cha upasuaji kulingana na miongozo husika, uzingatiaji wa kuweka taarifa za wagonjwa wanaopatiwa huduma za upasuaji (Documentation), pamoja na kulinda usalama wa mgonjwa na watoa huduma” alisema Bi. Kassanga.

Hata hivyo, Bi. Kassanga ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha watumishi juu ya utoaji wa huduma kwa kuzingatia Maadili, Miiko, Uadilifu, ikiwa ni Pamoja na uvaaji wa Sare maalumu za chumba cha upasuaji kulingana na miongozo husika, uzingatiaji wa kuweka taarifa sahihi za wateja wanaopatiwa huduma (Documentation), pamoja na kulinda usalama wa mgonjwa na watoa huduma” alisema Bi. Kassanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *