THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Jumla ya watahiniwa 5147 waliohitimu katika vyuo mbalimbali, wanatarajiwa kufanya Mtihani wa usajili na leseni unaoratibiwa na Baraza la uuguzi na ukunga Tanzania (TNMC) katika vituo vilivyotengwa kwenye mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Iringa, Tabora, Mwanza na Arusha.

Hilo limebainishwa na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa, mjini Kibaha mkoani Pwani, alipokutana na waandishi wa habari.

Usajili amesema mtihani huo utafanyika Ijumaa ya Disemba 20, 2024, ambapo kati ya watahiniwa 5147, wanajumuisha wahitimu ngazi ya Astashahada 86, Stashahada 4498, Shahada ya Uuguzi 537, Shahada ya Ukunga 11 na Shahada ya Uuguzi katika Utaoji dawa za usingizi na ganzi 11.

Aidha, Bi. Mtawa ameongeza kwa kuwataka watahiniwa wa Mtihani wa kada za Uuguzi na Ukunga, Kujiepusha na vitendo vya udanyanyifu wakati wa kufanya mtihani kwani atakayebainika kufanya hivyo atakabiliwa na adhabu ya kufutiwa matokeo ya Mtihani huo.