THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Waziri wa Afya Mhe. Jenesta Mhagama (Mbunge) amefanya uteuzi na kuzindua Baraza jipya la Uuguzi na Ukunga Tanzania(TNMC) lenye jumla ya   wa wajumbe 12 baada ya wajumbe wa Baraza la awali kumaliza muda wao

Uteuzi wa wajumbe 12 wa Baraza ni kwa Mujibu wa kifunga namba 5 – (1) cha Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 ambacho kimempa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Afya kufanya uteuzi wa wajumbe wa Baraza.

Aidha, wajumbe wateule watahudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu tangu kuteuliwa kwao.

Wajumbe hao ni Pamoja na;

1.Prof.Lilian Mselle,- Mwenyekiti ambaye ni Muuguzi mwandamizi,na na Mhadhili kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili, Shule ya Uuguzi.

(2). Dkt. Bankanie Vicent, Mjumbe anawakilisha waalimu wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma

(3) Bw. Alexander Baluhya Mjumbe-anayewakilisha Chama cha wauguzi Tanzania, kutoka Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Kabanga (4) Bi. Hilda Ndambalilo Mjumbe- Anawakilisha wauguzi wakuu wa mikoa ni muuguzi mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,

(5) Bi. Brenda Kitali Mjumbe- anawakilisha Wauguzi wakuu kutoka Hospitali za Rufaa, anatoka Hospitali ya KCMC,

(6) Bw. Sulle Samwel, Mjumbe- anawakilisha wauguzi kutoka Hospitali binafsi, anatoka Hospitali ya Haydom Manyara.

Wajumbe wengine ni; (7) Bi.Tumaini Lawrence, mjumbe- kutoka kwenye jamii anatoka Tanzania Association of Women Certified Accounts, (8) Bi. Ziada Sellah, mjumbe-Muuguzi mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, anatoka Wizara ya Afya Dodoma (9)

Bi. Ruhama Masanika, mjumbe-anawakilisha wauguzi ngazi ya cheti(EN) kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma,

(10) Wakili Bavoo Junus, mjumbe kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,

(11) Dkt. Alfred Sabahene, mjumbe- Kutoka kwenye jamii, kutoka Chuo Kikuu cha ST John Dodoma na

(12) Dkt. Fabian Byesigwa mjumbe- Anawakilisha taaluma nyingine,ni kutoka ofisi ya RMO  Mkoa wa mara.

Mh.Waziri amezindua baraza jipya na kuwapa wajumbe nyenzo za utekelezaji majukumu yao ambazo ni Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010 na Kanuni zake Pamoja na miongozo mingine.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TMNC ni mamlaka ya kisheria inayosimamia wanataaluma na taaluma za uuguzi na ukunga Tanzania, Chini ya Sheria ya Uuguzi na ukunga ya mwaka 2010 na kanuni zake (The Nursing and Midwifery Act 2010) ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini zinakiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.