THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Akizungumza na TNMC Habari akiwa ofisini kwake jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma TNMC Bi.Happpy Massenga amesema Mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma ni mchanganyiko wa shughuli mbali mbali za mafunzo anayopata mtaaluma ili kujenga umahiri na kuimarisha uwezo wake wa kutoa huduma bora. Mafunzo haya yanajumuisha kujifunza kila siku mambo mbalimbali katika eneo la kazi kutokana na uhitaji, changamoto zilizopo au uwepo wa mambo mapya (updates) katika taaluma na huduma kwa ujumla.

Mafunzo haya ni takwa la kisheria kwa wataalamu kufanya maendeleo endelevu ya umahiri wao wa kitaaluma kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010, Kanuni yake Kifungu cha 6 (28)(1) cha Kanuni ya mafunzo ya mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Training Regulations, 2010)

Bi. Massenga amefafanua lengo la Mafunzo ya kujiendelni kitaaluma kwa wauguzi na wakunga yameandaliwa ili kuwawezesha kufanya maendeleo endelevu ya umahiri wao wa kitaaluma ikijumuisha;

Kuboresha matokeo ya mgonjwa anayehudumiwa,Kurekebisha Makosa mengi yanayofanywa na wataaluma kwa sababu ya kukosa umahiri, ujuzi duni na mtazamo usiofaa dhidi ya taaluma na Makosa mengine yanatokana na uwepo wa teknolojia mpya katika huduma za Afya ambayo watendaji hawajaoneshwa au kujifunza.

Kwa Upande wake msimamizi wa Mafunzo hayo Bi. Mwajuma Mutabazi amebainisha Umuhimu wa mafunzo ya kujiendeleza kuwa ni Kukidhi mapungufu yaliyobainishwa katika ujuzi na maarifa ya mtaaluma binafsi na Taasisi kwa ujumla, Kumwongezea Muuguzi/Mkunga maarifa,ujuzi pamoja na kumpa mtazamo mpya (Knowledge,Skills and Attitudes) katika utoaji wa huduma, Kumwezesha Mtaaluma kutoa huduma bora kwa wateja wake zinazoendana na wakati, Huwawezesha wataaluma kukabiliana na changamoto mbalimbali za kuibuka kwa magonjwa, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa haraka wa sayansi na teknolojia, Huinua kiwango cha kufiri na kufanya maamuzi ya kisayansi katika utoaji wa huduma, Humsaidia mtaaluma kukidhi takwa la Kisheria na kuweza kuhuisha leseni yake.

Bi. Mwajuma amesema, Muda wa Mafunzo ya kujiendeleza yamegawanyika katika sehemu tatu ambapo alama 2- 40 zimetolewa moja, Mafunzo ya muda mfupi kuanzia saa moja mpaka mwezi
Pili, Mafunzo ya muda wa kati kuanzia miezi 3 hadi 6
Tatu ni  Mafunzo ya muda mrefu kuanzia mwaka mmoja na kuendelea.

Hata hivyo, kutakuwa na Maboresho katika taratibu za mafunzo ( CPD logbook) ambapo, Kuanzia mwaka 2023 marejea ya mwongozo wa mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma yalifanyika ili kuendana na miongozo ya Wizara hivyo kupelekea kufanyika ambapo, Mtaaluma anatakiwa kupata alama 20 kila mwaka kutoka maeneo mbalimbali ya kujifunza katika mchanganuo ulioonyeshwa katika kitabu cha kuweka kumbukumbu (CPD Logbook) na Jumla ya alama za mafunzo anazotakiwa kupata mtaaluma ili kuhuisha Leseni yake ni 60 ndani ya miaka mitatu (2023 hadi 2025)

Ikumbukwe kuwa, Mafunzo ya CPD yanapatikana kwa njia kadhaa yapo yale ambayo yanapatikana eneo la kazi ( non-accredited) ambayo mtaaluma anayapata kila siku eneo lake la kazi na yanapangwa na wataaluma wenyewe yakilenga kuboresha hali ya utoaji wa huduma na huduma kwa ujumla. Yanachukua asilimia 50 sawa na alama 30 ambapo mtaaluma atatakiwa kupata alama 10 kwa mwaka Pili, Mafunzo yaliyoratibwa na kupata itibathi ( Accredited CPD modules)  haya yameandaliwa na wadau mbalimbali kuanzia eneo la utoaji wa huduma na wanaosimamia miradi. Yanachukua asilimia 30 sawa na alama 18 ambapo mtaaluma atatakiwa kupata alama 6 kwa mwaka na Tatu, Mafunzo yanayopatikana kwa njia ya mtandao ( Online CPD) haya yanatolewa kupitia mtandao – mtaalamu anatakiwa kusoma maeneo yanayoongeza umahiri katika utoaji wa huduma. yanachukua asilimia 20 sawa na alama 12 ambapo mtaaluma atatakiwa kupata alama 4 kwa mwaka. Mtaaluma atasoma kupitia application ya WCEA (https://engagement.wcea.education/tnmc) na National e-leaning platform – ya Wizara ya Afya