Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania anawatangazia Watahiniwa wote wa kada za Uuguzi na Ukunga waliofanya Mtihani wa Usajili na Leseni tarehe 20.12.2024 na kufaulu kuwa, Mahafali ya 13 ya kutunuku Vyeti vya Usajili na Leseni yanatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 21.03.2025 kuanzia Saa 1:00 Asubuhi katika Ukumbi utakaotangazwa hapo baadae.
Hivyo, watahiniwa wote wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wa Mahafali ya 13 kwa kujisajili kupitia Tovuti ya Baraza www.tnmc.go.tz kuanzia leo tarehe 06.03.2025.
Kwa ufafanuzi Zaidi wasiliana nasi kwa namba; 0736 006060.