Kila ifikapo tarehe 19 machi ya kila mwaka Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Huadhimisha miaka siku ya kuanzishwa kwa taasisi hii.
Mwaka huu TNMC inatarajia kuadhimisha miaka 72 tangu kuanzishwa kwake mnamo 19 machi 1953 kwa kutembelea na kutoa misaada ya kibinadamu katika kituo cha watoto walemavu cha Mlali kilichopo jijini Dodoma.
Lengo kubwa la kuadhimisha hivyo ni kurudisha shukrani kwa jamii kama Taasisi ilivyo na wajibu wa kutoa huduma bora kwa watanzania.
Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.