Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, anawataarifu wauguzi na wakunga wote waliopata sifa za kusajiliwa na Baraza baada ya kufaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 20.12.2024 kuwa, Mahafali ya 13 ya kutunuku Vyeti vya Usajili na Leseni yanatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 21.03.2025 kuanzia Saa 01:00 Asubuhi katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha UDOM (Chimwaga Hall) uliopo Jijini Dodoma.
Aidha, kila mwanamahafali anatakiwa kuthibitisha ushiriki wake kwa kujisajili kupitia Tovuti ya Baraza www.tnmc.go.tz na kuhudhuria bila kukosa.
Wanamahafali wote mnaelekezwa kuzingatia mambo yafuatayo;
Kuvaa Sare ya Kitaaluma “Professional Uniform” iliyoidhinishwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga kama ifuatavyo: –
• WANAWAKE- Gauni au Suruali na Blauzi rangi nyeupe ndefu.
• WANAUME- Kaunda suti- Shati la rangi nyeupe na suruali rangi ya dark blue
• VIATU- Vinavyofunika miguu na siyo vya wazi, viwe vya rangi nyeusi, nyeupe au brown.
Kitambulisho cha Indexing, NIDA au Kitambulisho cha mpiga kura chenye picha ya mhusika/kinachomtambulisha.
NB: Sandozi au Kandambili haviruhusiwi.
