THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania leo 19 Machi 2025 limefanya maadhimisho ya miaka 72 Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1953.

Maadhimisho hayo ya kihistoria leo yamefanyika kwa kutembelea kituo cha watoto wenye ulemavu cha Mlali kilichopo wilayani Kongwa Dodoma.

Akizungumza katika hotuba yake kaimu Msajili TNMC Bi. Irene Chilewa amesema katika kipindi cha miaka 72 Baraza limepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi wauguzi na wakunga walisajiliwa ambapo na wenye madara mbalimbali ya elimu na hata nangazi ya Uzamivu PhD ambao jumla yao wamefikia taklibani 54,000, tofauti na miaka 72 iliyopita, kujenga mfumo wa TEHAMA, ujenzi wa ofisi za Baraza la Kibaha Mkoani Pwani na unaoendelea Jijini Dodoma.

“katika kuadhimisha siku ya Baraza tumekuwa tukitoa misaada na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii ambapo leo tumeleta mahitaji ya watoto yenye thamani ya Milioni Tano” amesema Bi. Irene

Naye Padri. Gaudence Aikaruwa, ambaye ni Mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na kutaja changamoto wanazokumbanazo katika malezi ya watoto hao ameshukuru Msaada huo ambao ni msaada mkubwa kwa sasa.

“Kituo kinawatoto zaidi ya 40 wanaolelewa mahali hapa, huu msaada utatusaidia sana Tunashukuru na Mungu awabariki” amesema Fr. Gaudence

Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya Kisheria inayosimamia wanataaluma na Taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Mwaka 2010 (The Nursing and Midwifery Act, 2010) ili kuhakikisha huduma zinazotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini Tanzania ni za kiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.