THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL


Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limekutana na wadau kwa lengo la kutoa taarifa ya namna mtaala mpya ulivyoandaliwa na namna utakavyotumika. kikao hicho kimefanyika leo katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Saalam.

Mtaala uliokamilika tangu mwaka 2022 kwa uwezeshaji wa wadau wa maendeleo (UNFPA) ambaye ameonyesha umuhimu wa kuendelea kuboresha mafunzo ya taaluma ya Uuguzi na Ukunga nchini.

Mtaala ya Uuguzi na Ukunga umeandaliwa kwa kuzingatia vigezo vilivyolinganishwa (Benchmarking) kupitia ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa kutokana na hali ya utendaji unaotakiwa kwa wauguzi na wakunga.

Pia Mtaala umezingatia tafiti na maamuzi ya vikao mbalimbali vya kitaaluma, ambapo kwa sasa taaluma ya Uuguzi na Ukunga inakuwa kwa kasi na kufikia ngazi ya ubobevu (PhD) ambapo wanahitajika wataalamu wenye sifa zinazostahili na kuwezesha wataaluma kujiendeleza.

Hata hivyo, mtaala wa Uuguzi na Ukunga umeshapata idhini na Baraza la Uuguzi na Ukunga na kupewa idhibati na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi umechelewa kuanza kutumika kutokana na baadhi ya wadau kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya taratibu za uandaaji wa mitaala.