Leo 15.04.2025 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Usajili na uorodheshwaji ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TNMC wanaketi kwa kikao cha kawaida cha robo ya tatu ambacho hufanyika kila robo mwaka kupitia utekelezaji wa majukumu ya Baraza kwa kurugenzi ya usajili na leseni.

Kamati hii inayoongozwa na Mwenyekiti ambaye pia ni mjumbe Baraza na Muuguzi mbobezi Bi. Brenda Kitali, inaratibiwa katibu ambaye ni Mkurugenzi wa kurugenzi ya usajili na Leseni ya TNMC Bi. Jane Mazigo.
Katika kikao cha leo, kamati inajadili agenda saba 07 zenye lengo la kuimarisha utendajika kazi wa Kurugenzi ya usajili na leseni na Baraza kwa ujumla wake.

Kamati ya Usajili na orodheshwaji (Registration and Enrolment Committee) ni moja ya kamati tano zilizoundwa chini ya kifungu namba 07 vifungu vidogo namba (01) na (02) vya The Nursing and Midwifery Act 2010 kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Baraza, jukumu kuu la kamati hii ni kuhakikisha wauguzi na wakunga wanaopewa idhini ya kutoa huduma za uuguzi na ukunga hapa Tanzania wanasifa zinazotakiwa kabla ya kupewa idhini na wanazidumisha sifa hizo wakati wote wa utoaji wa huduma
