
Leo 24.04.2025 Wajumbe wa kamati ya Elimu na Maendeleo ya taaluma ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TNMC wanafanya kikao cha kawaida cha robo ya tatu leo katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi za Baraza Jijini Dodoma.
Kikao hicho ambacho hufanyika kila robo mwaka kwa lengo la kupitia utekelezaji wa majukumu ya Baraza kwa upande wa Kurugenzi ya Elimu na Maendeleo ya taaluma.
Kamati hii inaongozwa na Mwenyekiti Dkt. Bankanie Vicent, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza na katibu wake ni Bi. Happy Massenga, ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu na Maendeleo ya Taaluma Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC)
kikao cha leo, kimebebwa na Agenda kuu Kumi (10) zenye lengo la kuimarisha utendaji kazi wa kurugenzi ya Elimu na Maendeleo ya Taaluma na Baraza kwa ujumla.
Ikumbukwe kuwa, kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ya mwaka 2010 kifungu cha 7(2)(b) Baraza limepewa jukumu la kuunda kamati ya Maendeleo ya Taaluma kwa lengo la kulisaidia Baraza katika mambo mbalimbali yahusuyo taaluma ya Uuguzi na Ukunga hapa nchini.

