THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Na Ezekiel M. Nyalusi (Iringa)

Chama cha Wauguzi Tanzania 11Mei 2025 walipiga kura kwaajili ya kupata uongozi mpya ambapo viongozi mbalimbali wamepatikana,

Uchaguzi huo uliofanyika katika Mkutano Mkuu wa chama uliofanyika Mkoani Iringa.

Akitangaza Matokeo hayo mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi huo Bwana Fidelis N. Gaakuba amesema kwa upande wa Uraisi  ameshinda Dr. Ezekiel Mbao kwa kura 90 kati ya kura 153, Makamu wa chama ameshinda Pendo Martha Joseph Shayo kwa kura 71 kati ya 153 huku nafasi ya Katibu mkuu akiwa Godfrey Chacha kwa kura 121 na katibu mkuu msaidizi wa chama ni Meshack Makojijo kwa kura 96.

Aidha, Mkutano huo umechagua viongozi wengine kwa ngazi ya Mhazini Mkuu ambaye ni Emiliana Mwakanyanga na Mhazini msaidizi akiwa ⁠Yohana Martin huku Nafasi ya katibu Mkuu Mwenezi akiwa ni Prosper Protas na katibu mwenezi msaidizi akiwa ni  Maria Mtweve

Uchaguzi huo hufanyika kwa mujibu wa sheria ya chama hicho huteua viongo wapya kila baada ya miaka mitatu na sasa Mkutano wa TANNA umeadhimia kufanyika tena mwaka 2026 katika jiji la Arusha.