THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Timu ya wauguzi na wakunga katika maeneo mbalimbali ya Ubobezi wakutana kwa lengo la kupitia mawanda ya kada ya Uuguzi na Ukunga Tanzania.

Akifungua kikao hicho muhimu kinachofanyika katika Ukumbi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi.Agnes Mtawa amewapongeza washiriki kwa kuitikia wito huo, huku akiwataka kufanya maamuzi sahihi katika eneo la mawanda ya taaluma hiyo.

Bi. Mtawa amebainisha kuwa, Lengo la kupitia Mawanda haya ni kuhakikisha yanaendana na matakwa ya taaluma ya Uuguzi na Ukunga kulinganga na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia kwa sasa.

Aidha, kikao hicho kimeandaliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga kwa kushirikiana na Mfuko wa kimataifa wa Idadi ya watu (UNFPA) na kinatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 27 hadi 29 Mei 2025.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania TMNC ni Mamlaka ya kisheria inayosimamia wanataaluma na taaluma za Uuguzi na Ukunga Tanzania, chini ya Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 na kanuni zake (The Nursing and Midwifery Act 2010) ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga nchini zinakiwango kinachokubalika na salama kwa jamii.