
Leo 04 June 2025 Muuguzi Mkuu wa Serikali Bi. Ziada Sellah amekutana na Muuguzi na Mkunga Edward Tumoyi ambaye mbunifu wa “Medical Robot Bed” ili kuweza kuifahamu kwa kina mfumo huo wa “Medical Robot Bed” namna unavyofanya na kutoa usaidizi katika utoaji huduma katima maeneo ya Afya.
Kikao kifupi hicho kilichofanyika katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa ofisi ya msajili Dodoma kimewakutanisha pia baadhi ya Wakurugenzi na wakuu wa sehemu katika ya Ofisi ya Muuguzi Mkuu wa Serikali, Makamu mstaafu wa chama cha wauguzi Tanzania (TANNA), Msajili TNMC na Mkurugenzi wa maendeleo ya Taaluma TNMC.
