Ofisi ya Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga “The Nursing and Midwifery Act, 2010” Kifungu cha (6) (a) na (o) inapenda kuwajulisha watahiniwa wote waliofanya Mtihani wa usajili na leseni tarehe 23.05.2025, kuwa matokeo ya Mtihani huu yametolewa leo tarehe 25 Juni, 2025 Jijini Dodoma.
Matokeo yanapatikana kupitia akaunti ya kila mtahiniwa iliyopo kwenye mfumo wa Kumbukumbu wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMCIS), kila mtahiniwa anatakiwa kupitia akaunti yake katika mfumo wa Baraza https://tnmcis.tnmc.go.tz ili aweze kuona matokeo yake.
Aidha, jumla ya watahiniwa 2842 walifanya Mtihani huu, ambapo watahiniwa 2080 (73%) wamefaulu mtihani huo na watahiniwa 762 (27%) walishindwa.
Baraza linawapongeza wale wote waliofaulu na kupata sifa za usajili na leseni, na linawaomba kusubiri tangazo la Mahafali ya kitaaluma, Kwa wale walioshindwa wajiandae kwa Mtihani mwingine.