THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Menejimenti ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) ikiongozwa na Msajili Bi. Agnes Mtawa leo Oktoba 1, 2025 imefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Ofisi ya Baraza (site visiting) kuangalia hatua za ujenzi wa Ofisi za Baraza.

Mradi huo utakaogharimu kiasi cha Shilingi billioni 1.8 za kitanzania unaotekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Strategic Business Solution Limited (SBS) unaendelea katika eneo la Medeli Jijini Dodoma ambapo kwasasa umefikia asilimia 89.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linajenga Ofisi Kuu Jijini Dodoma hii ni baada ya maelekezo ya Serikali ya kuzitaka Taasisi zote za Umma kuhamia Makao Makuu ya nchi, awali Ofisi kuu za TNMC zilikuwa Mjini Kibaha mkoani Pwani.