Ofisi ya Msajili inapenda kuwataarifu Wauguzi na Wakunga wahitimu wa Shahada za kwanza za Uuguzi na Ukunga wanaotarajia kujiunga na mafunzo ya Utarajali Mwezi Novemba 2025, kuwa dirisha la maombi kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania https://tnmcis.tnmc.go.tz/ litafunguliwa kuanzia tarehe 13.10.2025 Saa 4:00 Asubuhi hadi tarehe 17.10.2025 Saa 6:00 usiku.
Ili kukamilisha maombi na kuchagua vituo, wahitimu wenye sifa wanatakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo.
Nakala ya cheti cha kuzaliwa
Namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)
Nakala za vyeti vya elimu ya sekondari (O-level na A- level)
Leseni hai kwa wanaojiendeleza (Upgrading)
Passport size yenye ukubwa wa 360x300mm, back ground ya light bluе
Indexing namba ya Baraza la Uuguzi na Ukunga.
Nawatakia utekelezaji Mwema
Imetolewa na
Agnes Mtawa
Msajili – TNMC
12.10.2025, Jumapili