THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA NURSING AND MIDWIFERY COUNCIL

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) anaufahamisha umma kwamba kikao cha Baraza cha (225) kilichoketi leo 11 Februari 2026 kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga “The Nursing and Midwifery Act, 2010” kifungu cha (6) (a) na (o), kimepitia na kuidhinisha matokeo ya Mtihani wa usajili na leseni uliofanyika 19 Disemba 2025 katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Tabora


Matokeo hayo yanapatikana katika akaunti ya kila mtahiniwa iliyopo kwenye mfumo wa Kumbukumbu wa Baraza (TNMCIS), hivyo kila mtahiniwa anatakiwa kuingia kwenye mfumo wenye anuani ya https://tnmcis.tnmc.go.tz ili aweze kuona matokeo.


Baraza linawapongeza wale wote waliofaulu na kupata sifa za usajili na leseni na kwa ambao hakufikia alama za ufaulu zinazokubalika, wajiandae kwa Mtihani mwingine.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano TNMC