Wahitimu wote wa kada za Uuguzi, Ukunga na Utaalamu wa dawa za usingizi na ganzi, wanaotarajia kufanya Mtihani wa Usajili na Leseni, mnatangaziwa kuwa dirisha la maombi litafunguliwa rasmi kuanzia Jumamosi ya tarehe 12.04.2025 hadi Jumatatu ya tarehe 12.05.2025.
Maombi yatafanyika kwa njia ya mtandao kwa kutumia mfumo Rasmi wa Baraza https://tnmcis.tnmc.go.tz/ muombaji kwa mara ya kwanza anatakiwa kujisajili na kulipia kiasi cha Tsh. 150,000/= na muombaji anayerudia atalipia kiasi cha Tsh. 75,000/=
Aidha, Mtihani unatarajiwa kufanyika tarehe 23.05.2025 hivyo kila muombaji anatakiwa kuzingatia taratibu zote za maombi kama ifuatavyo : –
Uwe umefaulu Mtihani wa kufuzu Mafunzo kwa Ngazi husika (Qualifying Examination),
Uwe na namba ya utambulisho (Indexing Number) kwa mujibu wa kifungu cha 14 (01) cha kanuni za mafunzo,
Kuweka picha sahihi (Passport Size 45mmX35mm) background iwe ya Lightblue,
Kujaza majina sahihi yanayoendana na vyeti vya kumaliza Elimu ya Sekondari,
Kufanya malipo na kuchagua kituo sahihi cha Mtihani kwa wakati
