MUHIMU:
Ofisi ya Msajili inawajulisha wote watakao ona majina yao katika orodha hii, kuwasiliana na Ofisi ya Msajili mara moja ili kukamilisha taarifa zao. Aidha, wale ambao hawajahuisha leseni zao kwa kipindi kirefu, Baraza linakusudia kuwachukulia hatua kama ilivyoelekezwa katika Kifungu cha. 38(1)(a) na (b) cha Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010
Orodha ipo katika makundi mawili kama ifuatavyo (click link to download)
ORODHA YA WANAOKUSUDIWA KUONDOLEWA (HAWAJABORESHA TAARIFA) hawa wanatakiwa kuwasiliana na Ofisi ya Msajili kwaajili ya kuboresha taarifa zao, wanatakiwa kutumia. Email: info@tnmc.go.tz kufanya mawasiliano.
ORODHA YA WANAOKUSUDIWA KUONDOLEWA KWENYE REJESTA (INACTIVE) hawa hawajahuisha leseni zao, zaidi ya Miezi sita watatakiwa kuhisha leseni zao ndani ya siku 30 tangu tangazo hili lilipotangazwa watakaoshindwa kuhuisha leseni zao kwa kipindi tajwa Baraza halitasita kuwaondo kwenye Daftari la Usajili.
Naomba kuwasilisha.
Asante.