Hayo ameyasema leo wakati wa kikao kifupi walichokiomba wanafunzi wa kada ya uuguzi na Ukunga wa chuo St. John na Ofisi ya Msajili kikao ambacho kimefanyika chuoni hapo jijini Dodoma.

Akitaja umuhimu wa usajili wa awali Msajili amesema ni Kurahisisha ufuatiliaji wa wanafunzi waliodahiliwa na wanaoendelea na mafunzo katika vyuo, Kurahisisha mchakato wa usajili baada ya kuhitimu mafunzo, Hurahisisha ufuatilia wa maendeleo ya mafunzo vyuoni na kutoa takwimu ya wanafunzi wanaostahili kufanya mtihani wa leseni na usajili na kujua hali ya udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Uuguzi na Ukunga

Aidha, Msajili amesisitiza kuwa, Usajili wa awali (student indexing) si kwa ajili ya kupata kibali cha kufanya mtihani wa Usajili na Leseni tu bali ni zoezi muhimu linalomwezesha mwanafunzi kufanyiwa uhakiki wa sifa za kujiunga na masomo ya Uuguzi na Ukunga kisha kupata/kutopata kibali cha kuendelea na masomo yake.
Hata hivyo, Wadahiliwa ambao orodha/taarifa zao hazijawasilishwa Baraza hawataweza kufanya usajili huu, Sambamba na hilo, mwanafunzi atapata kadi ya usajili wa awali (indexing card) itakayotumika kwa kipindi chote cha uanafunzi na wakati wa mtihani wa Usajili na leseni.
Ikumbukwe kuwa, utaratibu wa kujisajili ni kuingia kwenye tovuti ya Baraza kwa kuandika neno TNMCIS au www.tnmc.go.tz Baada ya kuingia kwenye ukurasa huu wa Baraza bofya TNMCIS login utaona ukurasa huu na Bofya “click here to register” kwa waombaji wapya ambao hawana akaunti Baraza Kwa sasa maombi mengi kupitia Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania yanafanyika kwa njia njia mtandao. Hivyo mwombaji anawajibika kuchagua ombi sahihi kwa wakati huo kama ambavyo ukurasa hapo juu unavyoonyesha.
Kumbuka: kwa wanafunzi wenye akaunti tayari kwenye mfumo wa Baraza hawatakiwi kujisajili tena bali wanatakiwa kuingia moja kwa moja kwenye mfumo (login) kwa kuweka barua pepe na nywila tu kisha kuendelea na kukamilisha maombi.