MAHAFALI YA TISA YA TNMC WAUGUZI, WAKUNGA WATABASAMU
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeandaa Mahafali kwa Wahitimu wote wa Kozi za Uuguzi na Ukunga waliofaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 07/9/2023, Mahafali haya yaliyofanyika katika Ukumbi wa “CATHEDRAL SOCIAL HALL”Jijini-Dodomayataambatana na utoaji wa Vyeti vya Usajili na Leseni.
TAARIFA YA MAHAFALI YA TISA YA KITAALUMA KWA WAUGUZI NA WAKUNGA.
Dodoma-Tanzania 09.01.2024. Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania anawaarifu Wahitimu wote wa Kozi za Uuguzi na Ukunga waliofaulu Mtihani wa Usajili na Leseni uliofanyika tarehe 07/9/2023, Kuwa Mahafali ya kutoa Vyeti vya Usajili na Leseni yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 16/1/2024 kuanzia Saa1:00 Asubuhi katika Ukumbi wa “CATHEDRAL SOCIAL HALL”Jijini-Dodoma Maelekezo ya kufika […]
TNMC: Wauguzi, wakunga na watarajali 134 wamenufaika na Mafunzo ya Maadili DSM
Jumla ya Wauguzi, wakunga na watarajali 134 wamenufaika na Mafunzo ya Maadili pamoja na uhamasishaji kuhusu Maadili katika Hospitali tatu ambazo ni Hosiptali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali tanzu ya Mloganzila na Hospitali ya Tumbi Kibaha Mkaoni Pwani.Mkurugenzi Ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga kutoka Idara ya Usajili, Leseni na Maadili Bi. […]
TNMC: Wauguzi, wakunga zaidi ya 200 wapigwa Msasa Mafunzo ya Sheria na Maadili Mkoani Morogoro.
Timu ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania imetoa Mafunzo ya Maadili na Sheria kwa Wauguzi na Wakunga 212 katika Halmashauri ya Mji Ifakara,Kituo cha Afya Kibaoni,Hospitali ya St Fransis,Hospitali ya Kilombero,Wauguzi kutoka Hamashauri Wilaya Mlimba na Chuo cha Uuguzi na Ukunga Edgar Maranta Mkoani Morogoro. Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni […]
TNMC imetangaza Matokeo ya Mtihani wa Usajili na Leseni Uliofanyika Tarehe O7.09.2023.
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) linatangaza Matokeo ya Mtihani wa usajili na leseni uliyofanyika tarehe 07.09.2023 Matokeo hayoyanapatikana kwenye akaunti ya kila Mtahiniwa kwenye mfumo wa Baraza (hppts://ww.tnmcis.go.tz). Matokeo haya yamechelewa kutangazwa kutokana na baadhi ya watahiniwa kukiuka taratibu za ufanyaji Mitihani ambazo zilizosababisha kufanyika uchunguzi ili kubaini chanzo cha ukiukwaji huo. Baraza […]
Mtihani wa Usajili na Leseni kufanyika Disemba 29,2023
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linatarajia kuendesha zoezi la Mtihani mapema siku ya Ijumaa 29/12/2023 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana, ambapo Jumla ya watahiniwa 4165 wamekidhi vigezo vya kufanya Mtihani huu, wakiwemo waombaji 3917 ambao wanafanya mtihani kwa mara ya kwanza na 248 wanaorudia, kati yao Wanaume ni 1647 na wanawake […]
Tangazo kwa Watahiniwa wa Mtihani wa Usajili na Leseni Disemba 29.2023
Ofisi ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania inawatangazia watahiniwa wote kufika vituo vya Mtihani wa usajili na leseni siku ya tarehe 28.12.2023 saa mbili asubuhi kwa ajili ya maelekezo. Aidha, kadi za indexin vitatolewa siku hiyo kwa ambao hawakuchukua awali, lakini pia namba za Mtihani zitabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo kituoni hapo na […]
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania latoa Msaada wa Kibinadam Hanang
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limepeleka misaada ya kibinadamu katika wilaya ya Hanang palipokumbwa na Maafa ya maporomoko ya tope, Desemba 3 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 89, majeruhi na wengine wakikosa makazi. Akikabidhi Misaada hiyo Bw. Augustino Mwita ambaye ni Mkaguzi wa ndani wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, amesema watumishi […]
TNMC Habari Yazuru Gazeti la Mwananchi.
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Ndimmyake Mwakapiso na Ezekiel Nyalusi, wameanza ziara ya siku saba ya kuzuru vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam. Katika siku ya kwanza leo Disemba 11/2023, kitengo kimefanya ziara katika chumba cha uchakataji wa Habari za Gazeti hilo mashuhuri Nchini. […]
Wataalamu wa Afya watakiwa kuzingatia Mafunzo ya chati Uchungu kupunguza vifo vya Mama na Mtoto
Wataalamu wa Afya wametakiwa kutumia taaluma na ueledi walionao kwa kuzingatia mafunzo ya chati uchungu ili kupunguza idadi ya vifo vya Mama na Mtoto ambavyo vimekuwa vikijitokeza. Hayo yamesema na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Daniel Mzee, wakati akizungumza na Madaktari pamoja na Wauguzi Wakunga katika mafunzo ya Chati Uchungu yanayofadhiliwa na USAID […]