KUSUDIO LA KUWAONDOA WAUGUZI NA WAKUNGA WENYE TAARIFA TATA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA USAJILI PAMOJA NA MFUMO WA TNMCIS

MUHIMU: Ofisi ya Msajili inawajulisha wote watakao ona majina yao katika orodha hii, kuwasiliana na Ofisi ya Msajili mara moja ili kukamilisha taarifa zao. Aidha, wale ambao hawajahuisha leseni zao kwa kipindi kirefu, Baraza linakusudia kuwachukulia hatua kama ilivyoelekezwa katika Kifungu cha. 38(1)(a) na (b) cha Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya Mwaka 2010 Orodha […]
CHUO KIKUBWA CHA KISASA CHA AFYA KUJENGWA DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga fedha katika Bajeti ya Mwaka 2024/25 kwa ajili ya kujenga chuo kikubwa na cha kisasa cha Afya – Mirembe cha uuguzi na ukunga kitakachokua na vifaa vya kisasa ambacho kitatoa wataala wa kutosha katika Sekta ya Afya. Waziri Ummy amesema hayo leo Juni 12, 2024 alipofanya ziara katika chuo […]
UJENZI WA OFISI ZA TNMC WAFIKIA 52%- DODOMA

Menejimenti ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) leo June 06, 2024 imefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Ofisi ya Baraza (site visiting) kuangalia hatua za ujenzi wa Ofisi za Baraza. Ujenzi huo unaotekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Strategic Business Solution Limited (SBS) unaendelea katika eneo la Medeli Jijini Dodoma ambapo […]
WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUIMARISHA MAHUDHURIO MAENEO YA KAZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amewawaagiza watumishi na wataalam wote wa Afya nchini kuimarisha mahudhurio kwa kuhakikisha wanakuwepo maeneo yao ya kazi kwa muda stahiki wanaotakiwa kuwapo ili kukabilina na majukumu yao na kuiepusha jamii na madhila ambayo yanaepukika. Dkt.Jingu ameyasema hayo Juni 9, 2024 wakati wa ziara yake ya kushtukiza […]
SERIKALI KUAJIRI WATUMISHIWA AFYA 10,112

Serikali imesema kuwa mwaka ujao wa Fedha itaajiri watumishi wa Afya 10,112 ili kukabiliana na upungufu wa watumishi hasa maeneo ya vijijini. Hayo yameelezwa bungeni, Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya Dkt. Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Khadija Taya […]
WAZAZI TENGENI BAJETI YA KUWANUNULIA TAULO ZA KIKE WATOTO WENU

Na WAF, ARUSHAWazazi na walenzi nchini wametakiwa kuhakikisha wanawawezesha watoto wa kike kila mwezi kupata vifaa vyao vyakujilinda na kuwa na hedhi salama katika muda husika. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molel wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la hedhi Salama Duniani ambayo Kitaifa yameadhimishwa Jijini Arusha. “Wazazi […]
BARAZA TNMC LA SIKILIZA TUHUMA ZINAZOWAKABILI WAUGUZI NA WAKUNGA LEO

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linaendesha Kikao cha kawaida cha Baraza la Uuguzi na Ukunga cha robo ya tatu, kinatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo tarehe 23 na 24/05/2024 kuanzia saa 03:00 asubuhi, katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma Kikao kinaendeshwa na Mwenyekiti wa Baraza Prof. Lilian Mselle, na wajumbe […]
WAZIRI MCHENGERWA: WAGONJWA WANAHITAJI FARAJA KUTOKA KWA WAUGUZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka wauguzi kula kiapo cha utoaji wa huduma bora ikiwa ni pamoja na kuwapa wagonjwa faraja na msaada wa saikolojia.”Msiondoke hapa mpaka mle kiapo cha kutoa huduma bora kwa niaba ya wauguzi wengine wote walioko kwenye vituo vya kutolea huduma […]
MAJALIWA: WAKUNGA ZINGATIENI WELEDI KWENYE UTOAJI WA HUDUMA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wakunga na wataalamu wengine wa afya nchini kufanya kazi kwa weledi na kuongeza bidii katika kutoa huduma kwa wananchi wanaowahudumia. Amesema kuwa kada zote za afya zinasimamiwa na miiko na maadili ya taaluma na miongozo iliyowekwa. “Hivyo basi kila mmoja ahakikishe anazingatia maelekezo mahsusi ya utendaji wa kazi.” […]
Heri ya siku ya wafanyakazi Duniani / Mei Mosi 2024

Wafanyakazi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) wameshiriki Katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Katika Maadhimisho hayo Mgeni rasmi ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo inasema “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao bora na kinga […]