TANZANIA TUMEJIPANGA KUUDHIBITI UGONJWA WA MPOX USIINGIE NCHINI MPOX – MHE. MHAGAMA

Serikali ya Tanzania imejipanga kuudhibiti ugonjwa wa Mpox usiingie nchini kwa kuimarisha uchunguzi kwa wasafiri kupitia huduma za Afya Mipakani ikiwemo bandari, nchi kavu na viwanja vya ndege, ili kubaini wasafiri wenye viashiria na dalili za ugonjwa huu na kuchukua hatua stahiki. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama Jijini Dodoma akizungumza na […]

Wizara ya Afya na Taasisi zake zatwaa Tuzo Maonesho ya Nanenane.

Wizara ya Afya na taasisi zake imetwaa Tuzo ya Wizara Mtambuka kwa kushika nafasi ya Tatu katika Maonesho Kimataifa ya Nane Nane 2024 Jijini Dodoma. Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekabidhiwa siku moja kabla yakukamilika kwa Maonesho hayo yaliyohitimishwa Agosti 10, 2024. Wizara […]

FAHAMU HAKI NA WAJIBU WA MGONJWA/MTEJA AKIWA KATIKA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.

Akizungumza na vyombo vya Habari katika Maonesho ya kimataifa ya Nanenane Jijini Dodoma Afisa Uhusiano Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) Ndugu Ezekiel Nyalusi amesema jamii ni vyema ikafahamu haki na wajibu wa mteja au mgonjwa pindi anapofika kupewa huduma za Afya katika kituo cha kutolea huduma. Ndugu Nyalusi amzeiainisha haki hizo kuwa ni: Kupatiwa […]

Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya ili kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi kutokana na maendeleo katika Sekta hiyo. Rais Dkt. Samia amesema hayo Julai 31, 2024 wakati akifunga Kongamano la kumbukizi la Hayati Benjamini […]

ZIFAHAMU KANUNI SABA ZA MAADILI YA UUGUZI NA UKUNGA NCHINI.

1. Heshimu Utu uhai.2. Pata idhini ya mteja kabla ya kutoa huduma.3. Timiza wajibu wako na kuwa tayari kuwajibika kwa matendo yako.4. Dumisha weledi na ujiendeleze kitaaluma.5. Uwe mwaminifu na kutoa huduma bila upendeleo.6. Shirikiana na watoa huduma wengine na kufanya kazi kama timu.7. Tunza siri za Mteja/ Mtu unaye mhudumia.

MTIHANI WA USAJILI NA LESENI KUFANYIKA AUGUST 23, 2024

Ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, inawatangazia   wahitimu wote wanaotarajia kufanya mtihani wa Usajili na Leseni, kuwa mtihani unatarajiwa kutafanyika tarehe 23/08/2024. Kwamba, Dirisha la maombi limefunguliwa lipo wazi toka tarehe 01/07/2024 na litafungwa tarehe 14/08/2024. Maombi yote yafanyike kupitia mtandao kwa kutumia mfumo wa Baraza www.tnmcis.tnmc.go.tz Waombaji wote mnajulishwa kuzingatia […]

UJENZI WA OFISI ZA TNMC DODOMA WAFIKIA 59.9%

Menejimenti ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) leo Julai 11, 2024 imefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Ofisi ya Baraza (site visiting) kuangalia hatua za ujenzi wa Ofisi za Baraza. Ujenzi huo unaotekelezwa na kampuni ya ujenzi ya Strategic Business Solution Limited (SBS) unaendelea katika eneo la Medeli Jijini Dodoma ambapo […]

slot gacor