TAARIFA JUU YA HITILAFU YA TOVUTI
SOMA JARIDA LA MWEZI FEBRUARI

DOWNLOAD HAPA
DKT. NTULI AIBUKA MSHINDI UKURUGENZI MKUU ECSA-HC

Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya kutoka Tanzania Dkt. Ntuli Kapologwe, ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati, na Kusini (ECSA – HC) na kuwashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo. Dkt. Ntuli anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Prof. Yoswa Dambisya wa Uganda […]
Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) wametembelea Ofisi ya Msajili -TNMC

Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) wametembelea ofisi ya msajili kufahamu utendaji kazi wake hususaji kuhusu sajili za wauguzi na wakunga hapa nchini wakiwa kama wadau katika utoaji wa huduma za kiafya hapa nchini. Madaktari Wasio na Mipaka (MEDECINS SANS FRONTIERES- MSF) ni akika nani? Hili ni Shirika lisilo la kiserikali na la […]
MSAJILI TNMC: INDEXING NI SUALA LA KISHERIA SI MATAKWA YA MTU BINAFSI

Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Agness Mtawa amewataka wanafunzi wote wa kada ya Uuguzi na Ukunga nchini kuhakikisha wanakamilisha usajili wa awali (Student Indexing) ili kuweza kutambulika na mfumo wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania. Hayo ameyasema leo wakati wa kikao kifupi walichokiomba wanafunzi wa kada ya uuguzi na Ukunga […]
UTARATIBU WA KUTOA MATOKEO YA MWISHO YA MITIHANI(RESULTS TRANSCRIPTS)
CHAMA CHA WAKUNGA TANZANIA (TAMA) CHAPATA ITHIBATI UTOAJI WA MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA (CPD)

Kwa niaba ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Mkunga Mbobezi na Mratibu wa Mafunzo ya Kujiendeleza Kitaaluma Bi. Mwajuma Mutabazi amekabidhi Cheti cha ithibati ya Moduli sita za mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma (CPD) eneo la huduma za dharula kwa wajawazito (Midwifery Emergency Skills Training) kwa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) ambapo amekitaka chama […]
TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA USAJILI NA LESENI ULIOFANYIKA 20.12.2024
BARAZA LATANGAZA MATOKEO YA MTIHANI WA WA USAJILI NA LESENI, UFAULU NI 64%

Akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani huu, tarehe 23 Januari, 2025, Jijini Dodoma, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Agnes Mtawa, amebainisha kuwa, jumla ya watahiniwa 5125 walifanya mtihani huu, ambapo watahiniwa 3281 (64%) wamefaulu mtihani na watahiniwa 1844 (36%) hawakuweza kufikia kiwango cha ufaulu kinachokubalika. Aidha, Matokeo hayo yanapatikana kwenye akaunti […]
WAUGUZI, WAKUNGA WAKUMBUSHWA JUU MAFUNZO YA KUJIENDELEZA KITAALUMA.

Akizungumza na TNMC Habari akiwa ofisini kwake jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma TNMC Bi.Happpy Massenga amesema Mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma ni mchanganyiko wa shughuli mbali mbali za mafunzo anayopata mtaaluma ili kujenga umahiri na kuimarisha uwezo wake wa kutoa huduma bora. Mafunzo haya yanajumuisha kujifunza kila siku mambo mbalimbali katika eneo la kazi […]