TNMC Yashiriki Mkutano wa ECSACON Lesotho
TNMC ikiwakilishwa na Msajili Bi. Agnes Mtawa, pamoja na maafisa waandamizi ambao ni Salome Kassanga na Irene Chilewa, imeshiriki Mkutano wa kimataifa wa kisayansi unaoratibiwa na jumuiya ya ECSACON nchini Lesotho kuanzia tarehe 11 hadi 13 Septemba 2024 kwa lengo la kubadilishana elimu, uzoefu na kuboresha utoaji huduma katika sekta ya Afya kwa nchi wanachama. […]
Msajili TNMC akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa TNMC mbele ya kamati ya Bunge.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchi Tanzania Bi. Agnes Mtawa akiwa na menejimenti yake, tarehe 06 Agosti 2024 aliwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Baraza mbele ya kamati ya Bunge inayosimamia sekta ya Afya na UKIMWI kupitia kikao kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge Bungeni Jijini Dodoma. Kamati hiyo ambayo iliongozwa na Mwenyekiti […]
“ONGEZENI KASI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA UUGUZI NA UKUNGA”-Waziri Mhagama.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Idara ya Uuguzi na Ukunga kuongeza kasi ya utoaji wa huduma za uuguzi na ukunga pamoja na kufuatilia ubora wa kazi hizo ili mwananchi apate huduma iliyobora. Waziri Mhagama amesema hayo Septemba 5, 2024 wakati wa kikao na Idara ya Uuguzi na Ukunga kwa ajili ya kujitambulisha na […]
Dkt. Ndugulile Rasmi ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.
Dkt. Faustine Ndugulile amechaguliwa Agosti 27, 2024 na wajumbe wa Kikao cha 74 cha WHO kanda ya Afrika kushika nafasi hiyo kuanzia Agosti 27, 2024 aliyepokea kijiti kutoka kwa Dkt. Matshidiso Moeti wa Bostwana ikiwa ni kwa mara ya Kwanza Tanzania inachukua nafasi hiyo. Dkt. Ndugulile ambaye ni Mbunge wa Kigamboni (CCM), Katika kinyang’anyiro hicho […]
Watahiniwa 3,099 wakidhi vigezo vya kufanya Mtihani wa Usajili na Leseni Agosti 23, 2024
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msajili TNMC Bi. Agnes Mtawa imeeleza kuwa Mtihani wa usajili na leseni unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2024. TNMC imefunga dirisha la usajili kwa watahiniwa wenye sifa za kufanya Mtihani huu, ambao hufanyika kwa Mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 Kifungu 6 (o) kwa lengo la […]
TANZANIA TUMEJIPANGA KUUDHIBITI UGONJWA WA MPOX USIINGIE NCHINI MPOX – MHE. MHAGAMA
Serikali ya Tanzania imejipanga kuudhibiti ugonjwa wa Mpox usiingie nchini kwa kuimarisha uchunguzi kwa wasafiri kupitia huduma za Afya Mipakani ikiwemo bandari, nchi kavu na viwanja vya ndege, ili kubaini wasafiri wenye viashiria na dalili za ugonjwa huu na kuchukua hatua stahiki. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama Jijini Dodoma akizungumza na […]
Wizara ya Afya na Taasisi zake zatwaa Tuzo Maonesho ya Nanenane.
Wizara ya Afya na taasisi zake imetwaa Tuzo ya Wizara Mtambuka kwa kushika nafasi ya Tatu katika Maonesho Kimataifa ya Nane Nane 2024 Jijini Dodoma. Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekabidhiwa siku moja kabla yakukamilika kwa Maonesho hayo yaliyohitimishwa Agosti 10, 2024. Wizara […]
FAHAMU HAKI NA WAJIBU WA MGONJWA/MTEJA AKIWA KATIKA KITUO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA.
Akizungumza na vyombo vya Habari katika Maonesho ya kimataifa ya Nanenane Jijini Dodoma Afisa Uhusiano Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC) Ndugu Ezekiel Nyalusi amesema jamii ni vyema ikafahamu haki na wajibu wa mteja au mgonjwa pindi anapofika kupewa huduma za Afya katika kituo cha kutolea huduma. Ndugu Nyalusi amzeiainisha haki hizo kuwa ni: Kupatiwa […]
Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira kwa kila Mwaka katika Sekta ya Afya ili kupunguza changamoto ya uhaba wa watumishi kutokana na maendeleo katika Sekta hiyo. Rais Dkt. Samia amesema hayo Julai 31, 2024 wakati akifunga Kongamano la kumbukizi la Hayati Benjamini […]
Mhe. Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya Wanariadha kwenye mbio za NBC Marathon Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Mapema Julai 28, 2024 ameongoza mamia ya Wanariadha kwenye mbio za NBC Marathoni zilizoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC Bank). Mbio hizo za Kilomita 42, 21, 10, 5 na Mbio maalum za Viongozi zimeanzia viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma na kuishi […]