
WAZIRI MHAGAMA MGENI RASMI WIKI YA AFYA KITAIFA
Maelfu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania leo wamejitokeza kwa wingi kushiriki kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa 2025, yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Mhe.Waziri wa Afya, Jenista Mhagama , akimuwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,