TNMC: Wauguzi, wakunga zaidi ya 200 wapigwa Msasa Mafunzo ya Sheria na Maadili Mkoani Morogoro.

Timu ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania imetoa Mafunzo ya Maadili na Sheria kwa Wauguzi na Wakunga 212 katika Halmashauri ya Mji Ifakara,Kituo cha Afya Kibaoni,Hospitali ya St Fransis,Hospitali ya Kilombero,Wauguzi kutoka Hamashauri Wilaya Mlimba na Chuo cha Uuguzi na Ukunga Edgar Maranta Mkoani Morogoro. Ikumbukwe kuwa, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania ni […]
TNMC imetangaza Matokeo ya Mtihani wa Usajili na Leseni Uliofanyika Tarehe O7.09.2023.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) linatangaza Matokeo ya Mtihani wa usajili na leseni uliyofanyika tarehe 07.09.2023 Matokeo hayoyanapatikana kwenye akaunti ya kila Mtahiniwa kwenye mfumo wa Baraza (hppts://ww.tnmcis.go.tz). Matokeo haya yamechelewa kutangazwa kutokana na baadhi ya watahiniwa kukiuka taratibu za ufanyaji Mitihani ambazo zilizosababisha kufanyika uchunguzi ili kubaini chanzo cha ukiukwaji huo. Baraza […]
Mtihani wa Usajili na Leseni kufanyika Disemba 29,2023

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania linatarajia kuendesha zoezi la Mtihani mapema siku ya Ijumaa 29/12/2023 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana, ambapo Jumla ya watahiniwa 4165 wamekidhi vigezo vya kufanya Mtihani huu, wakiwemo waombaji 3917 ambao wanafanya mtihani kwa mara ya kwanza na 248 wanaorudia, kati yao Wanaume ni 1647 na wanawake […]
Tangazo kwa Watahiniwa wa Mtihani wa Usajili na Leseni Disemba 29.2023

Ofisi ya Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania inawatangazia watahiniwa wote kufika vituo vya Mtihani wa usajili na leseni siku ya tarehe 28.12.2023 saa mbili asubuhi kwa ajili ya maelekezo. Aidha, kadi za indexin vitatolewa siku hiyo kwa ambao hawakuchukua awali, lakini pia namba za Mtihani zitabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo kituoni hapo na […]
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania latoa Msaada wa Kibinadam Hanang

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limepeleka misaada ya kibinadamu katika wilaya ya Hanang palipokumbwa na Maafa ya maporomoko ya tope, Desemba 3 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 89, majeruhi na wengine wakikosa makazi. Akikabidhi Misaada hiyo Bw. Augustino Mwita ambaye ni Mkaguzi wa ndani wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, amesema watumishi […]
TNMC Habari Yazuru Gazeti la Mwananchi.

Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Ndimmyake Mwakapiso na Ezekiel Nyalusi, wameanza ziara ya siku saba ya kuzuru vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam. Katika siku ya kwanza leo Disemba 11/2023, kitengo kimefanya ziara katika chumba cha uchakataji wa Habari za Gazeti hilo mashuhuri Nchini. […]
Wataalamu wa Afya watakiwa kuzingatia Mafunzo ya chati Uchungu kupunguza vifo vya Mama na Mtoto

Wataalamu wa Afya wametakiwa kutumia taaluma na ueledi walionao kwa kuzingatia mafunzo ya chati uchungu ili kupunguza idadi ya vifo vya Mama na Mtoto ambavyo vimekuwa vikijitokeza. Hayo yamesema na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Daniel Mzee, wakati akizungumza na Madaktari pamoja na Wauguzi Wakunga katika mafunzo ya Chati Uchungu yanayofadhiliwa na USAID […]
Ummy aagiza Daktari na Muuguzi kuchukuliwa hatua

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametaka Mabaraza ya Madaktari na Wauguzi kuwachukulia hatua Mganga na Muuguzi waliosababisha kifo cha mjamzito Mariam Zahoro kilichotokea Kituo cha Afya Kabuku, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Mwalimu amesema Mariam hakufariki kwa ajili ya kukosa kiasi cha shilingi 150,000, bali ni kwa ajili ya uzembe wa baadhi ya wahudumu wa […]
TNMC YAWAPIGA MSASA WAUGUZI,WAKUNGA NAMNA YA KUSHIRIKI UTOAJIHUDUMA KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI – NDANDA.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania limeendesha Mafunzo ya namna ya kushiriki utoaji huduma katika chumba cha upasuaji kwa Wauguzi na Wakunga katika Hospitali ya St. Benedict iliyopo Ndanda – Halmashauri ya Masasi,Mkoani Mtwara ambapo washiriki walikuwa ni Wauguzi na Wakunga, wataalamu wa dawa za usingizi na ganzi pamoja na Madaktari wa upasuaji. Akitoa mafunzo […]
MSAJILI WA BARAZA LA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA ATUA MAFIA

MAFIA- Timu ya Maofisa wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania wakiongozwa na Msajili wa Baraza Bi. Agnes Mtawa, mapema leo wamezuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa kisiwa cha Mafia kwa lengo la kujitambulisha kabla ya kuanza zoezi la utoaji Elimu ya Sheria na Maadili kwa wauguzi na wakunga wa Wilaya ya Mafia iliyopo […]